Baadhi ya wakulima wameiomba serikali kuhakikisha inawasajili sambamba na kuwapatia namba za usajili ili waweze kupata pembejeo za kilimo kupitia mfumo wa ruzuku ya serikali hususan katika kipindi hiki kuelekea msimu mpya wa kilimo.

Wakulima hao kutoka katika baadhi ya vijiji vya Musomo mkoani Mara wamesema licha ya serikali kuwasisitiza kujisajili kwenye mfumo huo lakini upatikanaji wa namba baada ya usajili umekuwa ni changamoto, Joyce Mwakalinga kutoka Musoma mkoani Mara anatueleza zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *