Serikali ya Tanzania imepeleka ujumbe maalum wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa Umoja wa Mataifa (UN), ambao umepokewa na Katibu Mkuu wa umoja huo Antonio Guterres.

“Tanzania imekuwa kitovu cha amani na mshikamano wa kijamii barani Afrika na duniani kote”, amesema Guterres akipokea ujumbe huo maalum uliowasilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje ya Nchi, Mahmoud Thabiti Kombo.

Guterres amesema Tanzania ikiwa kama ishara ya amani barani Afrika, ilijaribiwa katika uchaguzi wa hivi karibuni wa Oktoba 29, 2025; huku Baraza la Umoja wa Mataifa (UNSG) likisisitiza umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa yenye maana na jumuishi, ili kushughulikia sababu kuu za matukio yaliyotokea na njia za kuyashughulikia ili yasijirudie.

Katika hatua nyingine, Guterres ameahidi kuwa Umoja wa Mataifa utaunga mkono kikamilifu juhudi zinazoendelea hivi sasa na hata baada ya Tume ya Uchunguzi kukamilisha jukumu lake.

✍ @abuuyusuftz
#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *