Mkuu wa Wilaya ya Butiama Thecla Mkuchika ameiagiza Mamlaka ya Maji Mugango-Kiabakari kupeleka huduma ya maji katika hospitali mpya ya wilaya hiyo, Kizurira Nyerere

Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dkt. Nangi Nangi ameiomba serikali kupeleka maji katika hospitali ya wilaya na vituo vya vingine vya afya vya wilaya hiyo.

Aidha, Dkt. Nangi amesema kuwa upatikanaji wa maji utawawezesha wahudumu wa afya kufanya kazi yao kwa ukamilifu wa hali ya juu, na kuongeza kuwa uhaba wa maji ni changamoto kubwa kwa vituo vya afya katika wilaya hiyo.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *