Serikali ya Mkoa wa Mtwara imeishauri Wizara ya TAMISEMI kuangalia namna ya kutoidhinisha vibali vya uhamisho kwa watumishi wanaoomba kuhama vituo vyao vya kazi ndani ya mkoa huo, hatua hii inalenga kuongeza ufanisi wa utendaji kazi wa watumishi na kuboresha huduma zinazotolewa na serikali kwa wananchi.
Hatua hiyo imebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, wakati akitoa taarifa ya mkoa kwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Reubern Kwagilwa, aliyeko ziarani mkoani humo.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi