Wananchi wa Mkoa wa Kagera wamesema ujenzi wa tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kampasi ya Kagera utafungua fursa mbalimbali za kibiashara na kuwasaidia wazazi kupunguza gharama za masomo kwa watoto wao, hususan gharama za usafiri na maisha ya nje ya mkoa.

Tawi hilo la chuo kikuu linatarajiwa kuwekewa jiwe la msingi mchana wa leo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Emmanuel Nchimbi hatua inayotajwa kuwa kichocheo cha maendeleo ya elimu na uchumi wa mkoa huo pamoja na maeneo ya jirani.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *