
Hapo jana viongozi wa nchi 10 za Ulaya pamoja na Rais wa Halmashauri Kuu ya umoja huo Ursula von der Leyen walikutana mjini Berlin kuunga mkono mazungumzo kati ya Marekani na Ukraine
Kwa upande wake, Rais wa Marekani Donald Trump alisema alikuwa na mazungumzo mazuri ya saa moja na viongozi hao wa Ulaya.
”Mengi yalihusisha vita vya Urusi na Ukraine. Na tulikuwa na mjadala mrefu na mambo yanaonekana kwenda vizuri. Lakini tumekuwa tukisema hivyo kwa muda mrefu, na ni jambo gumu.”
Trump pia amesema ahadi za usalama kwa Urusi na Ukraine ilikuwa miongoni mwa masuala yaliyojadiliwa na majadiliano yake yalikuwa mazuri.