Waziri wa Kilimo, Daniel Chongolo, ameonya juu ya hatari ya mashambulizi ya kihalifu ya mtandaoni kwenye mifumo ya kifedha, akiuagiza uongozi wa Benki ya Ushirika nchini (COOP Bank) kuimarisha ulinzi wa mifumo yake ya kidigitali ili kuzuia mianya inayoweza kutumiwa na wadukuzi.
Chongolo amesema kuwa usalama wa mifumo ya utoaji huduma za kifedha ni jambo la msingi katika kulinda uwekezaji uliofanywa na Serikali pamoja na wanahisa wengine, akisisitiza kuwa dosari yoyote ya kiusalama inaweza kusababisha hasara za kifedha na kuporomoka kwa imani ya wateja.
Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa huduma ya malipo ya kidigitali ya COOPESA, inayolenga kurahisisha miamala ya kifedha ndani na nje ya nchi.
✍ Ahmady Ali Mramba
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates