
Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR mchafuko hayo yanasambaa kwa kasi na kusababishwa ufurushwaji mkubwa wa watu ambao wengi wanakimbilia nchi jirani za Burundi na Rwanda.
Huko Bujumbura Burundi maelfu ya wakimbizi wanaowasili UNHCR inasema wamepatiwa hifadhi baada ya kukimbia machafuko nchini mwao.
Innocent Chubaka kutoka shirika la UNHCR aliyeko katika kambi ya muda ya Mugara katika jimbo la Rumonge nchini Burundi anasema “Niko hapa kwenye kambi ya Maghara, katika Mkoa wa Bujumbura, kando ya jimbo la Rumonge, ambapo tumepokea idadi kubwa ya wakimbizi wa Congo waliokuja kwa mitumbwi hatarishi kupitia ziwani”
Ameongeza kuwa Hali ni mbayá, mbayá sana, wanaishi katika mazingira ambayo wameacha kila kitu na wanauhitaji wa vitu vingi mno. Kwa hiyo ningependa kutoa ombi la msaada wa dharura ili kutuwezesha sisi kuwapatia mahitaji baada ya kuwahamishia katika kambi ya Makombe”
UNHCR yahitaji msaada
UNHCR imesema takriban wakimbizi 64,000 wameshawasili Burundi na idadi ya wanaowasili inatarajiwa kuendelea kuongezeka.
Kwa sasa shitrika hilo linahitaji msaada ili kuweza kukidhi mahitaji makubwa ya msingi ya wakimbizi hao wanaowasili na jamii zinazowapokea.
Tangu 1 Desemba, jimbo la Kivu Kusini limeshuhudia kuongezeka kwa mapigano kwa kiwango kikubwa zaidi katika mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC tangu mwanzo wa mwaka huu wa 2025.