#HABARI: Kuelekea mchezo wa Derby ya mashabiki wa Simba SC na Yanga SC, Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Edward Mpogolo amewakabidhi pesa taslimu kiasi cha shilingi milioni tano, umoja wa mashabiki wa vilabu vya soka nchini, ambao wameungana pamoja kuhamasisha Watanzania kuunga mkono timu za taifa, kuelekea michuano ya AFCON kupitia Tamasha la mashabiki Derby ambalo linatarajia kufanyika Desemba 21, 2025.
Akizungumza wakati akiwakabihi kiasi hicho cha pesa ikiwa ni katika kuunga mkono jitihada zao, katika kuhamasisha umoja na uzalendo katika michezo Mpogolo amesifu wazo hilo, akisisitiza upekee wake katika kuwaleta pamoja Watanzania.
Mpogolo amesema dhamira ya umoja na uzalendo, iliyooneshwa na vijana hao, ni jambo la kuigwa na jamii kwa ujumla hivyo kama Serikali hawana budi kuwaunga mkono katika jambo hilo.
Aidha, amewataka viongozi wa vilabu vyote nchini, kuwaunga mkono mashabiki hao katika tamasha hilo, linalolenga kuleta hamasa kwa Watanzania, kuelekea michuano ya AFCON.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania.