#HABARI: Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Ndg. Juma Hokororo, amesema Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 137 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu katika Shule ya Msingi Kituma, iliyopo Kata ya Mbulumbulu, akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya sekta ya elimu kwenye wilaya hiyo.
Ndg. Hokororo amesema kati ya fedha hizo, shilingi milioni 86 zimetolewa kupitia mradi wa BOOST kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa madarasa matatu pamoja na ofisi, hatua itakayosaidia kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa wanafunzi na walimu katika shule hiyo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania