
Rais Trump alianza hotuba yake kwa kutaja orodha ndefu ya kile anachokiona kama mafanikio yake katika mwaka wake wa kwanza madarakani.
Alisema licha ya kuirithi nchi ikiwa katika hali mbaya kutoka kwa mtangulizi wake Joe Biden, lakini wamefanikiwa kuleta mabadiliko chanya kuliko rais mwingine yoyote katika historia ya Marekani.
Miongoni mwa masuala aliyoyagusia kwa kifupi ni uhalifu, uhamiaji vita dhidi ya dawa za kulevya na kuliimarisha tena jeshi la Marekani.
Amegusia pia suala la kupunguza bei, ambalo linaibua wasiwasi mkubwa miongoni mwa Wamarekani na kuahidi taifa hilo kuimarika kiuchumi mwaka ujao katika kiwango ambacho ulimwengu haujawahi kushuhudia.