Dar es Salaam. Katika dhama za ukuaji wa teknolojia ya mawasilianoAirtel Tanzania  imezindua teknolojia mpya ijulikanayo kama Voice over LTE (Airtel VoLTE), hatua ambayo inaendelea kuonesha dhamira yake kuendelea kutoa huduma za mawasiliano ya kisesa yaani kwa wateja wake nchini kote.

Kupitia teknolojia hio, wateja wa Airtel walio na simu janja zenye uwezo wa 4G na 5G wataweza kupiga na kupokea simu kupitia mtandao wa 4G na 5G kwa ubora wa juu na kasi zaidi, huku wakifurahia mawasiliano bora kama wako katika mazungumzo ya ana kwa ana.

Tekinolojia hio inawapa wateja uwezo wa kupiga simu huku wakiendelea kutumia intaneti bila usumbufu, jambo linaloongeza ufanisi wa huduma za kidijitali. Mbali na ubora wa sauti, teknolojia hio pia inachangia kuokoa matumizi ya betri ya simu yako na kuifanya idumu zaidi na kutoisha haraka, kuongeza kasi ya kuunganisha simu na kuruhusu wateja kubadilika kutoka simu ya sauti kwa urahisi na pia bila gharama ya ziada. Mara tu huduma inapowashwa katika kifaa au simu yako yenye uwezo wa Airtel VoLTE, mteja huanza kufurahia huduma hiyo moja kwa moja bila kuhitaji usajili.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Charles Kamoto, alisema kuwa kuanzishwa kwa teknolojia hioni hatua muhimu iliyopo ndani ya dhamira ya Airtel katika kuhakikisha watanzania wanaendelea kupata huduma bora na za kisasa. “Uzinduzi huu ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuendeleza uwekezaji mkubwa na ubunifu ili kuhakikisha mawasiliano yanapatikana kwa kasi, ubora na uhakika—kwa kifupi, mawasiliano,” amesema Kamoto.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Uhandisi wa Mtandao wa Airtel Tanzania, Prosper Mafolealisisitiza kuwa Airtel inaendeleza kuboresha na kusambaza miundombinu ya kisasa ya mawasiliano ili kuzidi kuboresha maisha ya mteja wa kawaida, wa kibiashara na wa taasisi. Alieleza kuwa Airtel VoLTE inaleta kiwango kipya cha ubora katika mawasiliano ya simu na ni sehemu ya mkakati mpana wa Airtel kuchangia kutimiza agenda ya serikali ya Tanzania ya kidijitali kutokana na kasi na ufanisi.

Uzinduzi wa teknolojia hii unaimarisha zaidi dhamira ya mtandao huo ya kukuza ujumuishaji wa kidijitali, kuongeza ubora wa huduma na kuhakikisha kuwa kila mteja, awe nyumbani, kazini au kwenye shughuli za biashara, anapata uzoefu wa mawasiliano ulio imara, wa kisasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *