Mkuu wa mkoa wa Iringa Kheri James ametoa masaa 24 kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi (OCD) wilaya ya Iringa kuhakikisha anawakamata wazabuni wote wanaohusika kusambaza vifaa vya ujenzi ktk mradi wa ujenzi kituo cha afya kata ya Mahuninga wilayani humo ambao wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwa uzembe na kusababisha mradi huo kuendelea kusuasua licha ya kwamba mradi huo ulipaswa kuwa umekamilika miezi mitano iliyopita.
Kuchelewa kukamilika kwa mradi huo kunaendelea kusababisha wananchi kwenye maeneo hayo kutembea mpaka KM 16 kufuata huduma za afya.