#HABARI: Wilaya ya Kaliua, mkoani Tabora, imetenga ekari elfu kumi na sita za mradi wa kilimo na ufugaji wa kisasa, kwa ajili ya vijana na wanawake mia mbili na hamsini wa wilaya hiyo, ambapo kwa sasa kila mmoja atapatiwa ekari tano usimamizi, elimu, pembejeo, zana za kilimo, na baadae pia wafugaji watawezeshwa, huku Serikali ikithibitisha kumpata mnunuzi wa mazao yatakayozalishwa ikiwa ni utekelezaji wa mkakati wa kuyainua kiuchumi makundi hayo.
ITV Didital imeshuhudia zana hizo za kilimo pamoja na mamia ya vijana hao wakiwa na shauku ya kujikwamua kimaisha kupitia kilimo na ufugaji, chini ya utekelezaji wa mradi wa kilimo wa jenga kesho iliyobora (BBT) ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kaliua, Dkt. Gerald Mongella anaweka bayana utayari wa Serikali katika kuwawezesha vijana hao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.