Valeria Caccavo kutoka shirika la Msalaba Mwekundu mjini Bukavu amesema kuwa mapigano yaliyotokea mwezi huu yamekuwa makali zaidi kuliko ilivyokuwa awali.

Shirika hilo limeongeza kuwa machafuko katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Kivu Kusini yanaendelea kusababisha vifo na kuwalazimisha maelfu ya wakaazi kuyakimbia makaazi yao kwa hofu ya usalama.

Tangu mwanzoni mwa Desemba, zaidi ya watu 100 wenye majeraha ya risasi wametibiwa katika hospitali zinazosaidiwa na Msalaba Mwekundu huko Kivu Kusini.

Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa karibu watu nusu milioni wameyahama makaazi yao katika jimbo la Kivu Kusini tangu mwanzoni wa mwezi huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *