#HABARI: Mamlaka ya uwekezaji na maeneo malumu ya kiuchumi Tanzania Kanda ya Magharibi, imepanga kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kutafuta soko la uhakika la zao la muhogo linalolimwa kwa wingi katika wilaya hiyo na kuuzwa ndani na nje ya nchi ikiwemo Uganda, Rwanda na Sudan Kusini licha ya wakulima kutopata faida kubwa kutokana na zao hilo kuuzwa kwa bei ya chini hivyo kumuacha mkulima katika hali ya umaskini.

Mbunge wa Jimbo la Kakonko Alan Thomas Mvano akizungumza wakati wa ziara ya kuwatembelea wafanyabiashara na wakulima wa zao la muhogo katika baadhi ya maeneo wilayani humo amesema kuwa ni wakati muafaka wa kutafuta soko la uhakika ili wakulima waweze kunufaika huku Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania Kanda ya Magharibi Erastos Murayi akisema kuwa ipo haja ya kutafuta masoko ya uhakika ili kumkomboa mkulima na Serikali kwa ujumla.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *