Serikali kupitia Wizara ya Afya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mpango wa bima ya afya kwa wananchi wote, unaotarajiwa kuanza kutekelezwa Januari 2026.

Chini ya mpango huo, kiasi cha Shilingi 150,000 kwa mwaka kitaiwezesha familia yenye hadi watu sita kupata huduma za afya, hatua inayolenga kupunguza gharama za matibabu na kuongeza upatikanaji wa huduma kwa wananchi wengi zaidi.
Wizara ya Afya imesema zoezi la uelimishaji linaendelea nchi nzima ili kuhakikisha wananchi wanauelewa mpango huo kabla ya kuanza rasmi kutumika.

Benson Eustace
Mhariri | @claud_jm

#UTV108 #AzamTVUpdates #AdhuhuriLive

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *