Katika mji wa Tunduma, mkoani Songwe, zaidi ya vijana 600 kutoka kabila la Wasafwa, lenye asili yake mkoani Mbeya, wamefanya matembezi ya kitamaduni na kufunga kwa muda barabara ya mjini Tunduma, wakicheza ngoma na kuimba nyimbo za asili ya Wasafwa, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kutimiza mwaka mmoja wa umoja wao.
Waandaaji wa tukio hilo wanasema lengo ni kuimarisha mshikamano, kuenzi utamaduni, na kuhamasisha amani miongoni mwa vijana.
✍Joyce Lyanda
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates