Wizara ya Ulinzi ya UAE ilitangaza mwisho wa uwepo wake nchini humo kwa hiari yake na kwa uratibu na washirika wake, kufuatia wito kutoka Riyadh na AdeWizara ya Ulinzi ya Muungano wa Falme za Kiarabu (Imarati) ametangaza kujiondoa kijeshi nchini Yemen baada ya ndege za Saudi Arabia kushambulia mamluki wake kusini mwa Yemen huku Aden ikiitaka Abu Dhabi iache kuunga mkono pande zinazopigana nchini Yemen.n wa kuacha kuunga mkono pande zinazopigana nchini Yemen.

Lakini Baraza la Mpito la mamluki wa Imarati huko Yemen limepinga hatua hiyo ya Abu dhabi na kusema kuwa, mashambulizi ya ndege za kijeshi za Saudia katika mji wa bandari wa Mukalla huko Yemen ni uvamizi na ni uchokozi rasmi.

Wataalamu wanasema kuwa, matukio hatari yanaendelea kutokea nchini Yemen hivi sasa, hasa baada ya tofauti kati ya Riyadh na Abu Dhabi kugeuka kutoka migogoro ya kimya kimya na kuwa mapambano ya wazi ya kisiasa na kijeshi, ambayo hatimaye yamepelekea ndege za Saudi Arabia kushambulia bandari ya Mukalla huko Hadramaut.

Wakati huo huo, muungano unaoongozwa na Saudia nchini Yemen umetangaza kwamba ulifanya shambulio la anga dhidi ya meli zilizobeba misaada ya kigeni katika bandari ya Mukalla kwa sababu meli mbili zilikuwa zimewasili Mukalla kutoka bandari ya Fujairah ya UAE bila ya idhini rasmi na zilizima mifumo ya ufuatiliaji wa bandari hiyo na zilishusha silaha, hatua ambayo inachukuliwa kuwa ni aina moja ya kuwasaidia kijeshi mamluki wa Imarati wanajiita Baraza la Mpito la Kusini, kwa lengo la kuutia kwenye matata makubwa zaidi mzozo wa Yemen.

Muungano huo ulithibitisha kwamba shambulio hilo lilifanywa kufuatia ombi la Rashad al-Alimi, mkuu wa Baraza la Uongozi la Yemen, na lengo lake lilikuwa ni kuwalinda raia wa Hadramaut mbele ya ukiukaji wa haki za binadamu unaofanywa na mamluki wa Muungano wa Falme za Kiarabu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *