Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Isarel, kwa kukiri kujiua kwa makumi ya wanajeshi wake, limekubali kuwa jumla ya wanajeshi 151 wamepoteza maisha katika mwaka huu wa sasa.
Kwa mujibu wa ripoti ya Pars Today, jeshi la utawala wa Kizayuni limetoa muhtasari wa takwimu za vifo vyake kwa mwaka 2025. Katika ripoti hiyo, ongezeko la vifo vinavyotokana na kujiua au kujinyonga limekuwa jambo lililovutia zaidi. Kulingana na takwimu hizo, zaidi ya wanajeshi 21 wa Israel wamefariki kwa kujiua, na idadi hii ndiyo kubwa zaidi ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Jeshi la utawala wa Kizayuni limetangaza kuwa ili kukabiliana na ongezeko la matatizo ya kiakili miongoni mwa wanajeshi wake, linapaswa kupanua huduma za matibabu.
Kuchapishwa kwa takwimu rasmi na jeshi la Israel kuhusu vifo vya mwaka 2025 kumeondoa pazia juu ya ukweli ambao kwa miaka mingi umefichwa mbele ya fikra za umma. Miongoni mwa aina mbalimbali za vifo vya kijeshi , kuanzia waliouawa vitani hadi waliokufa kwa maradhi au ajali, ongezeko la visa vya kujiua limekuwa jambo la linaashiria kina cha mgogoro ktika jeshi katili la Israel. Tukio hili si suala la mtu binafsi au la kisaikolojia pekee, bali ni kioo cha migogoro ya kimuundo na kisiasa katika utawala haramu wa Israel; mgogoro ambao umeingia katika tabaka mbalimbali za jeshi na jamii ya Israel, na sasa umejitokeza kwa sura ya takwimu rasmi.
Moja ya sababu za kuongezeka kwa kujiua katika jeshi la Israel inapaswa kuchambuliwa katika muktadha wa mashinikizo yanayotokana na vita vya kuchosha na visivyo na kikomo dhidi ya Wapalestina na eneo zima. Wanajeshi wa Kizayuni wanatekeleza majukumu yao katika mazingira ambayo hakuna mwanga wa mwisho wa mapigano unaoonekana, wala hawafahamu sababu hasa ya vita.
Hali hii, sambamba na kukabiliana kila siku na upinzani wa wananchi na ukatili wa kimuundo, imewaweka wanajeshi wa Kizayuni katika hatari ya kuchoka kiakili na kuhisi upweke wa maisha. Kama msemaji wa jeshi la Kizayuni alivyokiri katika ripoti yake ya hivi karibuni, viwango vya kujiua vimefikia kiwango kinachohitaji kuingilia kwa upana katika huduma za afya ya akili; kukiri kunakoonyesha kuwa mgogoro huu umevuka kiwango cha mtu binafsi na sasa umegeuka kuwa tatizo la taasisi.
Hali hii, sambamba na kukabiliana kila siku na upinzani wa wananchi na ukatili wa kimuundo, imewaweka wanajeshi wa Kizayuni katika hatari ya kuchoka kiakili na kuhisi upweke wa maisha. Kama msemaji wa jeshi la Kizayuni alivyokiri katika ripoti yake ya hivi karibuni, viwango vya kujiua vimefikia kiwango kinachohitaji uingiliaji wa dharura katika huduma za afya ya akili; kukiri kunakoonyesha kuwa mgogoro huu umevuka kiwango cha mtu binafsi na sasa umegeuka kuwa tatizo la taasisi.

Katika muktadha huu, ni lazima kuzingatia nafasi ya moja kwa moja ya vita vya Gaza na athari zake. Vita vya Gaza havikuwa na gharama za kijeshi pekee kwa utawala wa Kizayuni, bali pia vimewaletea wanajeshi wake mzigo mkubwa wa kisaikolojia na kiroho.
Urefu wa vita na kutojulikana mwisho wake, sambamba na mauaji makubwa ya Wapalestina huko Gaza, hususan wanawake na watoto, pamoja na shinikizo la fikra za umma duniani, ni miongoni mwa sababu kuu zilizochangia kuongezeka kwa kujiua miongoni mwa wanajeshi wa Kizayuni.
Zaidi ya hayo, vita vya siku 12 vilivyoanzishwa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Iran vilipiga pigo kubwa kwa morali au motisha ya wanajeshi wa Kizayuni. Wanajeshi wengi walilazimishwa kushiriki katika mapigano hayo, na kushindwa kwao kulidhoofisha kwa kiwango kikubwa ari ya wanajeshi wakiwemo wa wa ngazi za juu, na kuwasukuma zaidi katika hali ya msongo wa mawazo na kukata tamaa.
Mbali na mashinikizo ya kisaikolojia, udhaifu wa kimuundo wa jeshi la Kizayuni pia umechochea kuongezeka kwa visa vya kujiua; kiasi kwamba jeshi hilo limebidi liweke zaidi ya maafisa elfu moja wa afya ya akili katika vitengo mbalimbali na hata kutuma timu za uingiliaji wa haraka kwenye maeneo ya vita. Hatua hii, badala ya kuwa ishara ya ufanisi, ni kielelezo cha kushindwa kuzuia na kusimamia matatizo ya kisaikolojia kwa wakati. Mmoja wa maafisa wa kitengo cha afya ya akili wa jeshi la Kizayuni alikiri kwamba baada ya operesheni ya ‘Kimbunga cha Al Aqsa’, mahitaji ya huduma za kisaikolojia yameruka kwa kiwango kikubwa na wanajeshi katika vitengo vingi wanakabiliwa na dalili za msongo wa mawazo na huzuni.
Kwa upande mwingine, udhibiti na usiri wa vyombo vya habari wa utawala wa Kizayuni kuhusu vifo vya kijeshi daima umekuwa sehemu ya siasa za kudhibiti fikra za umma. Lakini kuchapishwa kwa takwimu rasmi za kujiua kunathibitisha kwamba ukubwa wa mgogoro umefikia kiwango ambacho hakiwezi tena kufichwa. Pengo hili kati ya simulizi rasmi na uhalisia wa mambo limeongeza kutokuaminiana kwa jamii ya Israel dhidi ya jeshi la Kizayuni.
Mbali na mashinikizo ya kisaikolojia yanayotokana na vita na mapigano ya kudumu, sababu za kiuchumi, kitamaduni na kijamii pia zina nafasi kubwa katika kuzidisha migogoro ya kisaikolojia miongoni mwa wanajeshi wa Kizayuni. Muundo wa kijeshi wa Israel, unaotegemea kwa kiwango kikubwa huduma ya lazima na ya muda mrefu, unaweza kusababisha hisia za kutokuwa na maana na uchovu wa kiakili kwa wanajeshi. Mazingira ya kazi ya kijeshi, yenye masharti makali na vikwazo vya mtu binafsi, pamoja na shinikizo za kijamii zilizopo katika jamii ya Israel, ikiwemo ukosefu wa usawa, matatizo ya kiuchumi na mvutano wa kitamaduni, yote pia yamechangia kuibuka kwa matatizo ya kisaikolojia.
Kwa upande mwingine, kutangazwa kwa takwimu hizi na utawala wa Kizayuni kunapaswa kuchukuliwa kama ishara ya kuporomoka taratibu kwa mshikamano wa kijamii na kisiasa wa utawala huo. Wanajeshi waliopoteza matumaini ni dhihirisho la mgogoro wa kina zaidi katika ngazi ya jamii; mgogoro unaotokana na sera za uvamizi na usalama zisizo na upeo. Hata kama jeshi la Kizayuni litajaribu kudhibiti hali hii kwa kupanua huduma za kisaikolojia, mradi misingi ya mgogoro , yaani kuendelea kwa uvamizi, vita na ukosefu wa dira ya kisiasa na kiuchumi , itaendelea kudumu, visa vya kujiua vitabakia. Ukweli huu, zaidi ya kuwa suala la kibinadamu, ni kipimo cha kisiasa kinachoonyesha kuwa utawala uliojengwa juu ya misingi ya ukatili na vurugu, mapema au baadaye utajikuta ukikabiliwa na kurejea kwa ukatili huo ndani yake.