
Nchini Gabon, Rais Brice Clotaire Oligui Nguema amesaini agizo tatu za kiraisi siku ya Alhamisi, Januari 1. La kwanza linamteua Hugues Alexandre Barro Chambrier kama Makamu wa Rais wa Jamhuri. La pili linampandisha Hermann Immongault hadi nafasi ya naibu kiongozi wa Serikali. La tatu linarasimisha muundo wa serikali mpya ya Gabon. Timu hii mpya ya serikali ina mawaziri 31, ikilinganishwa na 30 katika serikali iliyopita, ikiwa na wanawake 10 na wanaume 21.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wa habari huko Libreville, Yves-Laurent Goma
Nchini Gabon, habari za kisiasa ziliongezeka kasi kuanzia siku ya kwanza kabisa ya mwaka. Mabadiliko ya kwanza yanayoonekana: Hermann Immongault anaondoka Wizara ya Mambo ya Ndani na kuchukua nafasi ya Naibu kiongozi wa Serikali, jukumu sawa na la Waziri Mkuu. Hermann Immongault alisimamia mchakato wa chaguzi zote wakati wa mpito, kwa hivyo anaonekana “kutuzwa” kwa usimamizi wake wa mchakato wa uchaguzi.
Watu wapya watatu wameteuliwa kwenye nafasi muhimu. Clotaire Kondja anachukua nafasi ya Wizara ya Petroli na Gesi. Thierry Minko ameteuliwa katika Wizara ya Uchumi, Fedha, Madeni, na Miliki ya Serikali. Kuhusu Marie-Edith Tassyla-Ye-Doumbéneny, balozi wa zamani nchini Ufaransa na mkuu wa zamani wa itifaki ya serikali, ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje.
Washirika kadhaa wanashikilia nafasi zao
Washirika kadhaa wa karibu wa rais Nguema wanashikilia nafasi zao. Ulrich Manfoumbi Manfoumbi anashikilia nafasi yake ya naibu kiongozi wa serikali akiwa na cheo cha Waziri wa Nchi. Jenerali Brigitte Onkanowa anabaki katika Wizara ya Ulinzi, huku Carmelia Ntoutoume akishikilia nafasi yake kama Waziri wa Elimu.
Hata hivyo, watu wawili mashuhuri wanaondoka serikalini: Henri Claude Oyima, naibu waziri wa Uchumi, Fedha, na Madeni, na Adrien Mougougou, Waziri wa Afya.