ARUSHA: WANANCHI na wafanyabiashara jijini Arusha wamesisitizwa kuimarisha usafi  kwenye maeneo yao ili kujikinga na magonjwa mbalimbali.

Aidha, makandarasi waliopewa zabuni za kukusanya taka wameagizwa kuhakikisha magari yao yanakuwa safi ili kuondoa kero kwa wananchi na watumiaji barabara ambazo taka zinaanguka badala ya kupelekwa eneo husika.

Rai hiyo imetolewa na Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Iranghe wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Ng’arisha jiji inayolenga kuhamasisha wananchi na wafanyabiashara kuhusu usafi wa mazingira akiwa eneo la Soko la Dampo Kata ya Sokoni One.

Amesema endapo wafanyabiashara na wananchi wakihasafisha mazingira magonjwa mbalimbali hayawezi kutokea hivyo suala la usafi si amri bali ni zoezi la kila siku katika kuhakikisha hata wateja wanapofika kununua bidhaa, kunakuwa pasafi.

“Zoezi la usafi si geni katika Jiji hili hivyo lazima tuhakikishe usafi unaimarishwa kila maeneo  yetu na hili ni zoezi mtambuka  na kusisitiza maendeleo yapo kwa wananchi na si ofisini hivyo hakikisheni mnaimarisha usafi kila siku katika maeneo yenu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *