Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia katika eneo la Nyarusura, Manispaa ya Musoma, mkoani Mara, kufuatia ajali ya moto ulioteketeza nyumba yao usiku wa kuamkia leo.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea wakati watu hao wakiwa wamelala, hali iliyosababisha kushindwa kujiokoa baada ya moto kuzuka ghafla.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana, huku vyombo vya usalama vikiendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha tukio hilo.
✍Augustine Mgendi
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates