Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameliomba Jeshi la Polisi nchini kuyapa kipaumbele makosa ya uhalifu mitandaoni,makosa ya barabarani yanayosababishwa na madereva bodaboda huku akisisitiza amri ya Waziri Mkuu,Dkt.Mwigulu Nchemba ya kuondolewa kwa pikipiki zilizojazana vituo mbalimbali vya polisi nchini baada ya kukidhi masharti ya kuruhusiwa kuondoka vituoni.

Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi Visiwani Zanzibar ambapo Naibu Kamishna Zuberi Chembela akitoa taarifa ya uhalifu kwa mwaka uliopita wa Ishirini na Ishirini na Tano.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *