#HABARI: Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, amepiga marufuku ucheleweshaji wa ujenzi wa jengo la kanda la TBS jijini Mwanza na kuagiza marekebisho ya haraka ya makosa ya kiuandisi yaliyojitokeza. Serikali imeshatoa zaidi ya Sh. Bilioni 12 kwa ajili ya mradi huo, hivyo Waziri amesisitiza kuwa sababu za ucheleweshaji zisizo na msingi hazitakubalika na mkandarasi lazima asimamiwe ipasavyo.
Ujenzi wa ofisi hii ya Kanda ya Ziwa ni sehemu ya mkakati wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuimarisha udhibiti wa ubora wa bidhaa nchini, ambapo miradi mingine kama hiyo inaendelea Dodoma na Arusha.
Kukamilika kwa jengo hili kutawezesha wajasiriamali wadogo na vijana wa kanda hiyo kupata huduma za viwango kwa urahisi, kupunguza gharama za usafirishaji, na kuchochea kasi ya kukuza viwanda.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Ashura Katunzi, amebainisha kuwa shirika hilo hutenga Sh. Bilioni 3 kila mwaka kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya maabara.
Lengo ni kuhakikisha kuwa ofisi hizo zinapoanza kufanya kazi, ziwe na vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kutoa huduma za ubora na viwango kwa haraka ili kuendana na kasi ya Serikali.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.