
Ni mwezi mmoja tu (tarehe 4 Desemba) tangu marais wa Rwanda na DRC wasaini makubaliano ya Amani ya Washington nchini Marekani chini ya uangalizi wa Donald Trump. Makubaliano hayo yalitiwa saini hapo awali na mawaziri wao wa mambo ya nje.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo, hali ya usalama mashariki mwa Kongo haijaimarika. Desemba imekumbwa na mashambulizi mapya kutoka kwa kundi lenye silaha la AFC/M23, linaloungwa mkono na Kigali, pamoja na mapigano makali na jeshi la Kongo na washirika wake.
Kulingana na ripoti ya wataalamu wanasema, kwa sasa asilimia 23.3 ya malengo ya Makubaliano ya Amani ya Washington yamefikiwa. Kiwango hiki kilikuwa tayari kimetambuliwa na utafiti huo tangu Novemba.
Kwa mujibu wa mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo Roger-Claude Liwanga, profesa wa sheria na mazungumzo ya kimataifa katika Chuo Kikuu cha Emory nchini Marekani, hali hii ya kudumaa inatia wasiwasi. Ambapo amesema “Maendeleo yaliyopatikana katika utekelezwaji wake yanasalia kuwa dhaifu, na sherehe rasmi ya kutia saini iliyofanyika katika mji mkuu wa Marekani mapema Desemba haikutoa msukumo mpya katika utekelezaji wake.
Waandishi wa ripoti hiyo kisha wanatoa mapendekezo kwa pande mbalimbali. Wanaitaka serikali ya Kongo kuharakisha utekelezaji wa operesheni dhidi ya FDLR na kuzingatia ushiriki wa MONUSCO, kikosi cha Umoja wa Mataifa. Pia wanaitaka Rwanda kutekeleza mpango wa kujiondoa na kuondoa hatua za ulinzi.
Watafiti hao wanaonya kuwa ikiwa hali itendelea namna ilivyo kwa sasa mkataba huo utapoteza uaminifu wake.