Wafugaji wa ng’ombe, mbuzi na kondoo mkoani Geita wameiomba Serikali, kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kufanya uchunguzi wa kina wa kisayansi ili kubaini chanzo cha magonjwa yanayoshambulia mifugo yao na kusababisha vifo, licha ya juhudi zao za kutoa tiba mbalimbali bila mafanikio.
Ombi hilo limetolewa mbele ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally, wakati wa mkutano maalum wa wadau wa mifugo na uvuvi uliofanyika wilayani Chato.
#AzamTVUpdates
✍Ester Sumira
Mhariri | @claud_jm