India. Wakitajwa waigizaji 10 bora kutoka India jina la Hrithik Roshan nyota anayefanya vizuri katika filamu za Bollywood lazima liwepo.

Licha ya mafanikio yake ipo simulizi ya maumivu, kejeli na masimango aliyokumbana nayo tangu akiwa mdogo. Hrithik Roshan alizaliwa mwaka 1974 akiwa na hali ya kimaumbile inayojulikana kitaalamu kama ‘Polydactyly’ yaani kuwa na kidole cha ziada, kwenye mkono wake wa kulia.

Kwenye mahojiano yake mbalimbali aliyowahi kuyafanya alisema akiwa shuleni alikumbana na udhalilishaji, kudhihakiwa na wanafunzi wenzake wakimcheka huku baadhi wakiogopa kukaa naye.

Aidha kwa muda mrefu, Hrithik alijifunza kuuficha mkono wake wa kulia ili wanafunzi wenzake wasione kidole cha ziada. Hata hivyo, changamoto zake hazikuishia hapo, mbali na hali ya vidole sita, alikumbwa na tatizo la kigugumizi  lililomtesa tangu utotoni.

“Nilikuwa mtoto asiyejiamini kabisa. Watoto waliniona tofauti, na hilo liliniumiza sana. Nilikuwa na kigugumizi kibaya sana. Kulikuwa na nyakati niliogopa hata kusema neno moja darasani,”

Licha ya changamoto hizo, Hrithik alipata msaada mkubwa kutoka kwa familia yake, hususani baba yake, Rakesh Roshan, ambaye ni mwigizaji na mtayarishaji maarufu wa filamu, kupitia mafunzo, mazoezi ya mara kwa mara. Hrithik alianza kupambana na kigugumizi pamoja na kujifunza kujiamini alivyo.

“Nilijifunza kwamba hofu yangu kubwa haikuwa watu, bali sauti ndani yangu, nashukuru baba yangu alinisaidia sana katika kuyashinda yote. Nadhani asingekuwa yeye mpaka sasa ningekuwa si chochote,”amesema Hrithik

Tofauti na matarajio ya wengi, Hrithik hakuwahi kuondoa kidole hicho kwa kufanya upasuaji, licha ya kupokea ushauri kutoka kwa mashabiki lakini aliamua kubaki nacho kama utambulisho wake.

“Kila mtu ana kitu kinachomfanya awe tofauti. Hivyo basi mimi kidole changu hichi cha sita ndio utambulisho wangu ambao kwa sasa haunifanyi tena kuwa mnyonge na badala yake unanifanya kuwa juu zaidi ya hapo awali.

“Niseme tu hii ni bahati na zawadi yangu kutoka kwa Mungu sababu si kila mmoja anayo ni wachache miongoni mwetu,”amesema

Hrithik Roshan aliingia rasmi katika ulimwengu wa filamu mwaka 2000 akionekana katika filamu ya ‘Kaho Naa… Pyaar Hai’ iliyompatia umaarufu mkubwa na tangu hapo alianza kuonekana katika kazi nyingine ambazo ziliandaliwa na baba yake ikiwemo Krrish, Dhoom 2, Jodhaa Akbar, Super 30, Kabh

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *