#MICHEZO: Mashabiki wa soka nchini wamejitokeza kwa wingi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam, wakijawa na shangwe na hamasa kubwa, kuipokea Timu ya Taifa, Taifa Stars, inayorejea kutoka Morocco baada ya kushiriki AFCON 2025.
Timu hiyo imeandika historia kwa kufuzu hatua ya 16 bora kwa mara ya kwanza katika historia ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika, hatua iliyowagusa Watanzania wengi na kuchochea mapokezi ya aina yake.
Mapokezi haya ni ishara ya kutambua mafanikio ya wachezaji na benchi la ufundi, huku Taifa Stars ikiendelea kuandika ukurasa mpya katika ramani ya soka la Afrika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.