
Marekani inadai meli hiyo ilikuwa ikisafirisha mafuta kwenda nchi kama Venezuela, Urusina Iran kinyume na vikwazo vya Magharibi. Urusi imekanusha madai hayo, ikisema meli yake ilikuwa ikisafiri kwa mujibu wa sheria za kimataifa na ilikuwa ikielekea katika bandari ya Urusi.
Wizara ya mambo ya nje ya Moscow imesema hatua hiyo “itasababisha mvutano zaidi wa kijeshi na kisiasa”, na kwamba ina wasiwasi na “utayari wa Washington kuibua migogoro ya kimataifa.”
Marekani imesema wafanyakazi wa meli hiyo wanaweza kufikishwa mahakamani, kauli ambayo wizara ya mambo ya nje ya Urusi imesema “haikubaliki kabisa.”