
Kugeuka kile alichokitaja kama “pango la majambazi” ambamo wasio na aibu wala hofu huchukua wanachokitaka, kwa maana ya nchi yenye nguvu kuamua kupora maeneo au kuitwaa nchi nzima isiyo na nguvu.
Katika matamshi makali yasiyo ya kawaida, ambayo yalionekana kurejelea vitendo kama vile kuondolewa madarakani Kiongozi wa Venezuela Nicolas Maduro mwishoni mwa wiki, Steinmeier ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema kwenye Kongamano huko mjini Berlin kwamba demokrasia ya kimataifa inashambuliwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.
Amesema tabia ya Marekani inawakilisha mpasuko wa pili kihistoria na kuvunjika kwa maadili ambayo mshirika huyo muhimu alisaidia kujenga utaratibu wa dunia uliopo.
Ingawa jukumu la rais wa Ujerumani kwa kiasi kikubwa ni la heshima tu, lakini maneno yake yana uzito fulani kutokana na kwamba Rais wa Ujerumani ana uhuru zaidi wa kutoa maoni kuliko wanasiasa.