#Habari: Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Halima Lutavi, imetangaza kuchukua hatua kali dhidi ya kampuni ya usafirishaji iliyohusika na kashfa ya usafirishaji wa dawa za kulevya. Katika hatua za awali, LATRA imesitisha huduma za mabasi yote ya mbeba abiria huyo, likiwemo gari namba AAM 297 CA lililokamatwa na dawa hizo, pamoja na magari mengine 12 yanayodaiwa kufanya kazi bila leseni. Aidha, mmiliki wa kampuni hiyo ameitwa rasmi ofisini kwa ajili ya mahojiano huku akisubiri hatua zaidi za kisheria na kikanuni kuchukuliwa dhidi yake.
Pamoja na hatua hizo, LATRA imetoa onyo kali kwa wamiliki wote wa mabasi, hususan yanayofanya safari za Kimataifa, kuacha mara moja tabia ya kubadilisha miundo ya magari yao kwa lengo la kuficha bidhaa haramu. Mamlaka imebainisha kuwa mabadiliko hayo ya miundo ni ukiukwaji wa taratibu na yanatumiwa kurahisisha uhalifu unaohatarisha usalama wa nchi. Hatua hii inalenga kuongeza umakini na uwajibikaji miongoni mwa wasafirishaji ili kuhakikisha sekta ya usafiri haitumiki kama daraja la uhalifu.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.