#HABARI: Wananchi wa Kata za Wendele na Mwendakulima wilayani Kahama wamempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea mradi wa umeme vijijini (REA) ambao umeanza kubadilisha maisha yao kiuchumi na kijamii. Shukrani hizo zimetolewa leo, Januari 10, 2026, mbele ya Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, wakati wa hafla ya kuwasha umeme katika vitongoji vya Majengo na Chapulwa, ambapo wakazi wameelezea kufurahishwa kwao na huduma hiyo muhimu iliyofikishwa karibu na makazi yao.
Katika ziara hiyo, Mhe. Salome Makamba amesisitiza kuwa Serikali imejipanga kuunganishia wananchi 1,700,000 nchi nzima huduma ya umeme ndani ya mwaka huu kulingana na maelekezo ya Rais. Akisisitiza kasi hiyo ya usambazaji, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini kutoka REA, Mhandisi Jones Olotu, amebainisha kuwa wakala huo unajiandaa kusaini mikataba mipya ya kusambaza umeme katika vitongoji 9,009 kote nchini ili kuhakikisha kila eneo linafikiwa na nishati hiyo kwa ajili ya kuchochea maendeleo.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.