
Maandamano dhidi ya utawala yanaendelea nchini Iran, ambapo nchi hiyo katika hali tete baada ya mamlaka kuamua kufunga intaneti nchini kote ili kuzuia usambazaji wa picha na uandaaji wa maandamano. Siku ya Jumatatu, Januari 12, maelfu ya Wairan walifurika katika uwanja mkubwa katikati mwa Tehran kuonyesha uungaji mkono wao kwa Jamhuri ya Kiislamu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mabalozi au wawakilishi kutoka Ujerumani, Ufaransa, Italia, na Uingereza, walioko Tehran, wameitishwa siku ya Jumatatu na mamlaka ya Iran, ambayo imelaani uungaji mkono ulioonyeshwa na nchi hizi kwa waandamanaji wa Iran, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran iliyorushwa na televisheni ya serikali.
“Tunathibitisha kuitishwa kwa mabalozi wa Ulaya,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imeliambia shirika la habari la AFP.
Bunge la Ulaya lawapiga marufuku wanadiplomasia na maafisa wa Iran kuingia katika majengo yake
Wanadiplomasia na maafisa wa Iran sasa wamepigwa marufuku kuingia katika Bunge la Ulaya,Spika wa bunge hilo, Roberta Metsola, ametangaza siku ya Jumatatu. “Wakati watu jasiri wa Iran wakiendelea kupigania haki na uhuru wao, nimeamua leo, Jumatatu, kupiga marufuku wafanyakazi wote wa kidiplomasia na wawakilishi wengine wowote wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuingia katika majengo yote ya Bunge la Ulaya,” amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Mamlaka ya Iran imezima mitandao ya intaneti na simu kote nchini tangu siku ya Ijumaa ili kupunguza usambazaji wa picha na taarifa kuhusu maandamano hayo.