
Akiwa na umri wa miaka 2, amezuru nchi karibia nane katika bara la Afrika, ziara iliyoanza Desemba 29, 2025.
Baadhi ya nchi alizotembelea ni Afrika Kusini, Angola, Botswana, Eswatini, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia na hatimaye Kenya. Ziara yake ya Kenya, iliyofanyika Jumapili, Januari 11, ilikuwa ya kipekee na ya kihistoria.
Rais wa Kenya, William Ruto, alimkaribisha rasmi kupitia video iliyosambaa sana kwenye mtandao wa kijamii wa TikTok, akisema: “Jambo, IShowSpeed. Karibu Kenya. Kenya si nchi nyingine tu, Kenya ni moyo, ni hisia, Kenya ni nyumbani.”
Akiwa Nairobi, IShowSpeed alionyesha mubashara (livestream) matembezi yake katikati ya jiji huku akifuatwa na makumi ya vijana.
Katika ziara yake alitembelea hifadhi ya taifa ya Nairobi, soko kubwa la jiji, kuzunguka mji kutumia helikopta, na kushuhudia kwa karibu utamaduni wa usafiri wa umma wa Kenya. Safari hiyo ilionesha kwa uwazi uchangamfu na nishati ya nchi.
Kupitia chaneli yake ya YouTube akiwa Kenya, IShowSpeed alipata wafuasi wapya zaidi ya 360,000, jambo lililomfanya kupata idadi ya wafuasi milioni 48 kwenye YouTube. Wakati huohuo, zaidi ya watu 200,000 walikuwa wakifuatilia mubashara chaneli yake alipokuwa katika ziara hiyo.
Akitoa shukrani zake kwa Wakenya, alisema: “Nawapenda sana nyote. Kenya, hatutoisahau kamwe.”
Lakini IShowSpeed ni nani hasa?