
Waziri wa maji nchini Morocco Nizar Baraka amesema nchi hiyo sasa imekabiliana na ukame wa muda mrefu baada ya mvua nyingi kunyesha majira ya baridi hivyo kuafikia viwango vinavyohitajika vya maji ya matumizi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa waziri Baraka Viwango vya mvua msimu huu vimepanda kwa asilimia 95 ukilinganisha na mwaka uliopita ambapo nchi hiyo iliandikisha asilimia 17.
Amesema kiwango cha wastani cha kujaza mabwawa kimepanda hadi asilimia 46, huku hifadhi kadhaa muhimu zikiwa zimejaa maji ya kutosha, mvua hiyo ikitoa afueni kwa sekta ya kilimo baada ya miaka mingi ya vikwazo vya maji.
Morocco imeshuhdia Miaka saba ya ukame mfululizo huku mabwawa mengi nchini humo yakikauka hali iliyochangia kupungua kwa uzalishaji wa ngano, idadi ya mifugo na kuathiri ajira nyingi katika sekta ya kilimo.
Katika kukabiliana na majanga kama haya, Morocco inalenga kusambaza asilimia 60 ya maji yake ya kunywa kutoka kwa maji ya bahari yaliyosafishwa ifikapo mwaka 2030.