Taarifa ya jeshi imeongeza kuwa wanamgambo 13 wameuawa wakati wa makabiliano hayo na watu wanne wamejeruhiwa.Wanamgambo wa kundi la Taliban la Pakistan wamekiri kuhusika katika tukio hilo wakisema pia kuwa wamezitia mikononi mwao silaha na droni za wanajeshi.

Islamabad inadai kuwa wanamgambo wa kundi la Taliban la Pakistan  wanahifadhiwa na utawala wa Taliban wa Afghanistan na wakisaidiwa na India. Nchi hizo hata hivyo zinakanusha shutuma hizo. Wanamgambo hao wa Taliban ya Pakistan waliongeza mashambulizi dhidi ya Islamabad tangu utawala wa Taliban ulipoingia madarakani Afghanistan mwaka 2021

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *