Rais Tshisekedi azuru Togo katika juhudi za kusaka amaniRais Tshisekedi azuru Togo katika juhudi za kusaka amani

Kulingana na taarifa kutoka ikulu ya rais wa Kongo, uhamasishaji wa hivi karibuni wa kidiplomasia unalenga kutumia juhudi za upatanishi zinazoongozwa na Waafrika badala ya zile za kimataifa. Tina Salama msemaji wa rais Felix Tshisekedi amasema kuwa hii haimaanishi kuwa mazungumzo ya Doha au ya Washington yameshindwa.

“Kwa nini Lomé? Kwa nini Luanda Tunabaki na Umoja wa Afrika, ambao ni mwanachama au mdau, kama tulivyosema mara kadhaa katika michakato ya Washington haswa. Mmoja wao ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika, na hata alitoa wito wa kusitisha mapigano mara moja wiki iliyopita, huku mwingine akiwa mpatanishi aliyeteuliwa na Umoja wa Afrika. Na kumbuka kwamba Rais João Lourenço alikuwa Washington kwa ajili ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya DRC na Rwanda. Hii inawakilisha aina ya mwendelezo katika juhudi za amani na utulivu katika sehemu ya mashariki ya nchi,” amesema Salama.

Wachambuzi wa siasa Kongo wanadhani kuwa kuna mambo mengi ambayo yanamsukuma Rais Tshisekedi kufanya hivyo. JOSEPHA MUSAMBA ambaye ni mtaalamu wa masuala ya makundi ya waasi na mchambuzi wa siasa za Kongo amesema “Ya kwanza hata kama rais Felix Tshisekedi anasema hawezi kuzungumza na waasi wa M23 lakini kiukweli wamekuwa wakizungumza huko Doha na kumekuwa duru nyingi sana

Picha ya pamoja | Joao Lourenco na Felix Tshisekedi
Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika na Rais wa Angola Joao Lourenco alipokutana na RAis Felix Tshisekedi katika kikao cha faragha wakati wa Mkutano wa 38 wa Umoja wa Afrika (AU), katika Makao Makuu ya AU huko Addis Ababa mnamo Februari 16, 2025Picha: Amanuel Sileshi/Fabrice Coffrini/AFP/Getty Images

Ni kusema kuwa hiyo imekuwa msemo lakini ukweli wa shamba la vita umebadilika. Ya pili inaweza kuwa kama njama ya Felix Tshisekedi kuwubaisha waasi wa M23 tubaki tunazungumza na vita inaendelea na yatatu kumekuwa na shinikizo nyingi kutoka umoja wa mataifa ili kuwepo na mazungumza ya taifa kwa kupata amani.”

Ingawa baadhi ya wachambuzi bado wanatilia shaka kuhusu nia ya Tshisekedi ya kujadiliana na waasi aliowafukuza, raia wengi wa Kongo waliozungumza na DW wanaona hili kama hatua inayowezekana kuelekea suluhisho la amani.

Wakati juhudi za kutafuta amani ya kudumu zikiendelea, hali ya usalama inazidi kuzorota mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokraia ya Kongo ambapo kumekuwa na mapigano kila kukicha baina ya waasi sio tu wa M23 katika eneo la mashariki mwa Kongo lakini pia mobondo katika magharibi mwa nchini na bakatakatanga katika eno la katikati mwa nchi hiyo. Maelfu kwa mamia ya familia zililazimika kukimbia makwao kwa hofu ya usalama huku wengi wakifariki dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *