
Kwa mujibu wa maafisa, vito kutoka makumbusho zaidi ya 20 nchini kote viliibiwa au kuharibiwa, na hasara inakadiriwa kufikia takriban dola za Kimarekani milioni 110.
Maeneo yaliyolengwa wakati wa mapigano yalikuw Makumbusho ya Ikulu ya Rais, Makumbusho ya Vikosi vya Ulinzi, Makumbusho ya Nyumba ya Khalifa, Makumbusho ya Etnografia, na Makumbusho ya Historia ya Asili katika Chuo Kikuu cha Khartoum.
Awali, Mamlaka zilisema kuwa baadhi ya vitu vilivyochukuliwa tayari vilivushwa kwa njia za magendo katika mipaka ya nchi hiyo na sehemu kubwa ya vito hivyo bado haijulikani ilipo.
Hata hivyo, tangu Aprili 2025, serikali ya Sudan imekuwa ikishirikiana na Interpol na UNESCO kurejesha mali za kitamaduni zilizoibiwa.
Septemba mwaka uliopita, UNESCO ilitoa tahadhari ya kimataifa ikionya nyumba za makumbusho, wakusanyaji, na nyumba za mnada kutochukua au kuuza mali za kitamaduni zinazotoka Sudan.
