#HABARI: Washiriki wa Kozi ya Kumi na Nne ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania kutoka mataifa saba duniani, yakiwemo Misri, Malawi, Rwanda, Burundi, Kenya, India na Tanzania, pamoja na wakufunzi waandamizi na maafisa wanadhimu wa chuo hicho, wameanza ziara ya siku sita ya mafunzo kwa vitendo mkoani Tabora, ili kulinganisha nadharia wanazojifunza darasani na utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya Serikali katika nyanja za uchumi, siasa na kijamii.
Kiwanda cha kutengeneza mashine za mkaa mbadala cha Kuja na Kushoka Tools Manufacture kilichopo Manispaa ya Tabora ni maeneo ambayo washiriki hao wametembelea ambapo Kaimu mkuu wa chuo hicho Brigedia Jenerali Charles Ndiege ameona kuna tija ya nchi katika kusimamia matumizi ya nishati safi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
