#HABARI: Mamlaka ya Udhibiti wa Nafaka na Mazao Mchanganyiko (COPRA) imekabidhi tani 2.9 za mbegu za mbaazi kwa uongozi wa Mkoa wa Songwe, zilizofanyiwa utafiti na taasisi ya TARI Ilonga. Hatua hii ni utekelezaji wa ahadi ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yenye lengo la kuanzisha rasmi kilimo cha zao hilo kama zao la biashara katika Wilaya ya Songwe, ikizingatiwa kuwa mkoa huo una mazingira mazuri yanayofaa kwa kilimo cha mbaazi.
Akipokea mbegu hizo, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Bwana Wilfred Myuyu, amewahakikishia wakulima kuwa mbegu hizo zitawafikia kupitia vyama vya ushirika (AMCOS) na kuwatoa hofu kuhusu soko. Amesema kuwa zao hilo litauzwa kupitia mfumo wa Stakabadhi Ghalani, ambao umekuwa mkombozi mkubwa kwa kuhakikisha wakulima wanapata bei nzuri na soko la uhakika la mazao yao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
-
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
