Daktari wa Magonjwa ya Binadamu, Isihaka Mahawi, amesema ugonjwa wa selimundu si ugonjwa unaoambukiza bali hurithiwa kutoka kwa …Daktari wa Magonjwa ya Binadamu, Isihaka Mahawi, amesema ugonjwa wa selimundu si ugonjwa unaoambukiza bali hurithiwa kutoka kwa …

Daktari wa Magonjwa ya Binadamu, Isihaka Mahawi, amesema ugonjwa wa selimundu si ugonjwa unaoambukiza bali hurithiwa kutoka kwa wazazi wote wawili, na huathiri chembechembe nyekundu za damu.

Amesema ugonjwa huo huwapata zaidi watoto walio chini ya miaka mitano, hasa katika kanda ya Ziwa na Pwani, maeneo yenye kiwango kikubwa cha malaria ambayo huongeza madhara kwa wagonjwa wa selimundu.

Daktari Mahawi amesema wagonjwa wa selimundu wanaweza kuishi maisha ya kawaida iwapo watapata huduma za afya kwa wakati, kula lishe bora yenye madini chuma, na kujikinga dhidi ya magonjwa, hususan malaria.

✍Ibrahim kilumbo
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *