
Sheria hiyo imepitishwa na bunge la Ukraine tarehe 13 Januari 2026, na haifuti tu kanuni zilizopitwa na wakati bali pia inafungua njia ya mageuzi makubwa ya sekta ya makazi kulingana na changamoto za sasa na ahadi za kimataifa za Ukraine.
Sheria hiyo inafafanua misingi ya kisheria, kiuchumi, kijamii na na sera ya makazi ya serikali kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wa haki ya kila mtu ya kupata makazi na matumizi bora ya rasilimali za nyumba nchini Ukraine.
Katibu Mtendaji wa UNECE apongeza hatua hiyo
Katibu Mtendaji wa UNECE, Tatiana Molcean, amepongeza hatua hiyo akisema “Wakati Ukraine ikiendelea kustahimili mashambulizi dhidi ya makazi na miundombinu yake, napongeza kupitishwa kwa sheria ya Kanuni za Msingi za Sera ya Makazi, ambayo ni ishara thabiti kwa jamii, jamii za wenyeji, wawekezaji, na washirika wa kimataifa kuhusu dhamira ya nchi hiyo katika mageuzi ya makazi. UNECE inajivunia kuisaidia serikali katika mchakato huu wote na inatarajia kuendelea kusaidia katika utekelezaji wake.”
Sheria hii inafuta Kanuni ya Makazi ya mwaka 1983, ambayo haikidhi tena mahitaji ya kisasa ya Ukraine. Katika kiini cha sera hiyo mpya ni kuanzishwa kwa mifumo ya kisasa ya utoaji wa makazi, makazi ya kijamii na ya gharama nafuu, pamoja na mifumo ya kifedha kama vile mikopo ya nyumba na ukodishaji.
Aidha, sheria inatabiri kuundwa kwa “Mfumo Unganishi wa Taarifa na Uchambuzi wa Makazi,” ambao utafanya tathmini ya mahitaji kuwa ya kidijitali na kuhakikisha uwazi.
Mageuzi haya yanalenga kuboresha mazingira ya kuishi kwa mamilioni ya raia, wakiwemo watu waliofurushwa makazi yao. Miongoni mwa kanuni za sheria hiyo ni upatikanaji wa huduma na ujenzi usio na vizuizi, ukiunga mkono mbinu jumuishi kwa watu wenye ulemavu.
Sera hiyo mpya inazingatia mbinu za kimataifa hususan Mkataba wa Geneva wa Umoja wa Mataifa kuhusu Makazi Endelevu, na inaendana na Malengo ya Maendeleo Endelevu SDGs, ya mwaka 2030.
