Fedha za Mixx Pesa zawawezesha washindi kiuchumiFedha za Mixx Pesa zawawezesha washindi kiuchumi

Kampeni ya Magifti ya Mixx Pesa imechangia kuimarisha hali ya kiuchumi kwa baadhi ya wananchi baada ya fedha zilizotolewa kwa washindi kuingia moja kwa moja katika matumizi ya kaya na biashara ndogondogo.

Akizungumza Januari 14, 2026 Ofisa  Mtendaji Mkuu wa Mixx by Yas, Angelica Pesha wakati wa hafla ya kuhitimisha kampeni hiyo amesema katika kipindi chote cha kampeni hiyo, kulikuwa na ushindi wa kila siku, wiki, ushindi wa msimu wa sikukuu pamoja na mshindi mkuu, ambapo fedha zilitolewa kwa wateja waliokuwa wakishiriki.

“Tumeona washindi wakitumia fedha hizi kwa mahitaji ya msingi, wapo waliolipa ada za shule za watoto wao, wengine wakaongeza mitaji ya biashara ndogondogo, hali iliyosaidia kupunguza presha ya gharama za maisha,” amesema Pesha.

Amesema kampeni hiyo imeongeza mzunguko wa fedha katika jamii kwa kuchochea matumizi ya bidhaa na huduma mbalimbali, ikiwemo bidhaa za rejareja, usafiri wa kila siku na huduma nyingine za kijamii.

Pesha amesema wamebaini  ongezeko la matumizi hayo limewanufaisha pia wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wauzaji wa rejareja, wasafirishaji na watoa huduma za kila siku.

“Hii ni ishara kuwa fedha zinapoingia kwa mwananchi wa kawaida, athari yake huonekana moja kwa moja kwenye uchumi wa jamii,” amesema.

Amesema licha ya kampeni hiyo kufikia tamati, tathmini inaendelea kufanyika ili kubaini maeneo ya kuboresha katika kampeni zijazo, akieleza kuwa mahitaji ya wateja hubadilika kulingana na hali ya uchumi.

Naye, mshindi wa Sh50 milioni, Yusuph Constantine amesema ushindi alioupata umemshangaza na kumfanya atambue kuwa licha ya nafasi za kushinda kuwa ndogo, bado zipo na zinaweza kumfikia mtu yeyote.

Amesema kupokea zawadi ya kiasi hicho cha pesa bila kufanya uwekezaji au maandalizi yoyote makubwa ni jambo kubwa kwake na limebadili kabisa namna anavyotazama promosheni zinazofanywa na kampuni mbalimbali.

“Kwa mtu ambaye umeishi maisha yako ya kawaida, hujafanya uwekezaji wowote mkubwa, halafu ghafla unapewa Sh 50 milioni hilo ni jambo kubwa sana na nimefurika furaha,” amesema Constantine.

Mkurugenzi wa Biashara Mixx by Yas, James Sumari amesema washindi  walichaguliwa kwa uwazi, huku ushindi wao ukitangazwa na kushirikishwa kwa umma kupitia majukwaa ya mtandaoni ili kuwapa motisha washiriki wengine kuendelea kushiriki.

Kwa mujibu wa Sumari, simulizi na ushuhuda kutoka kwa washindi zimeonesha jinsi kampeni hiyo ilivyobadili maisha yao, ambapo baadhi waliweza kulipa ada za shule kwa wakati, wengine waliwekeza kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo, huku wengine wakitumia zawadi hizo kusafiri au kuanzisha biashara ndogondogo.

“Kuna washindi waliofunga mwaka kwa kishindo na wanafungua mwaka mpya wakiwa na matumaini mapya. Ushuhuda wao unatupa moyo wa kuendelea kuendesha kampeni kama hizi kwa uwazi na kwa lengo la kuwainua wananchi kiuchumi,” amesema Sumari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *