
Waganda wanapiga kura leo Alhamisi hii, Januari 15, kumchagua rais na wabunge. Uchaguzi huu unafanyika katika hali ya sintofahamu wakati jeshi na mtandao vikizua taharuki na katika hali ya mvutano mkubwa wa kisiasa na usalama.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Yoweri Museveni, 81, rais kwa miaka 40, anatafuta muhula wa saba na anatumai kubaki madarakani. Yowri Museveni aanagombea uchaguzi huo wa urais na wagombea saba, akiwemo mwanamuziki wa zamani Bobi Wine, 43—ambaye jina lake halisi ni Robert Kyagulanyi—ambaye anaonekana kuwa mpinzani wake mkuu.
Tayari wapiga kura wameanza kuwasili katika vituo vya kupiga kura ingawa asubuhi hii bado ni taratibu.
Maafisa wa usalama wamesambazwa katika maeneo mbalimbali wakati raia wanaamkia siku ya kupiga kura. Maafisa wa usalama pia wanajishughulisha na kuondoa picha za wagombea mbalimbali ambazo zilikuwa zimesambazwa wakati wa kampeni.
Waandishi wa habari waliokita kambi katika eneo hilo wameshuhudia maafisa wa usalama katika karibu kila pembe ya jiji la Kampala wakiwa kwenye magari huku wengine wakiwa wanatembea kwa miguu.
Mbali na wagombea hawa wawili wakuu, wagombea wengine sita wanashiriki kinyang’anyiro hicho katika taifa lenye takribani watu milioni 45. Tume ya uchaguzi inasema kuna wapiga kura milioni 21.6 waliojiandikisha.
Wachambuzi wengi wanaamini Museveni atabaki madarakani, lakini akiwa na umri wa miaka 81, inadaiwa amekuwa akitegemea zaidi vyombo vya usalama kulinda mamlaka yake. Mwanawe, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ndiye kamanda mkuu wa jeshi, hali inayozua maswali kuhusu kuingiliwa kwa uchaguzi.
