MTWARA: BAADHI ya wakulima wa zao la korosho katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara wamesema kupitia fedha za malipo ya korosho watahakikisha watoto wote waliyochaguliwa kwenda shule wanawanunulia sare.

Yamebainishwa hayo wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala kuhusu kukagua miundombinu ya elimu kwenye halmashauri zote tisa mkoani humo.

Aidha, miundombinu hiyo iliyotembelewa kwenye halmashauri  hiyo ikiwemo shule ya sekondari nandonde pamoja na shule ya msingi mahuta mjini, miradi iliyogharimu zaidi ya Sh milioni 192.

Baadhi ya wakulima wazazi kwa jumla Siajabu Lupanda mkazi wa kijiji cha mahuta mjini kwenye halmashauri hiyo amewashauri wazazi wenzake kuwa wajitahidi kuwanunulia sare watoto kwasababu fedha za malipo ya korosho wanazo.

Amesema serikali inasisitiza kuwa watoto wapokelewe shule hata kama hawana sare lakini wazazi nao walichukulie jambo hilo kwa umuhimu wake badala ya kuchukuwa fedha hiyo kucheza mpeano au upatu kuanzia Sh 50,000 hadi 100,000 kwa kila mwezi.

“Shule zinapofungwa ripoti inapokuja inaandikwa suala la sare kwahiyo kipindi hiki chote mzazi unatakiwa ufanye maandalizi ili shule zinapofunguliwa mtoto awe ameshapata sare”amesema Siajabu

Mkulima na mzazi mwingine katika kijiji hicho,  Niya Bushiri ameendelea kuwasisitiza wazazi hao ambao bado hawajawanunulia watoto sare wazingatie hilo ili kumfanya mtoto ajione kuwa yuko sawa na wenzake.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Kitongoji cha Amani Mahuta Mjini, Rashidi Buruani amesema baada ya wanafunzi waliyoandikishwa na wakapokea agizo la mkuu huyo wa mkoa kuhusu mtoto yoyote aliyeandikishwa hata kama hana sare apokelewe shule wamewapa muda maalumu wazazi wa kutekeleza jambo hilo.

Hata hivyo kutokana na kujitokeza kwa baadhi ya watoto ambao hawana sare na wameripoti shule,  mkuu huyo wa mkoa anaendelea kusisitiza watoto hao wapokelewe huku taratibu  zingine zikiendelea mtoto akiwa anaendelea na masomo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *