Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma imemfikisha mbele ya Baraza la Maadili Mkuu wa Idara ya Mipango wa Halmashauri ya Wilaya Mbogwe, mkoani Geita, Alex Manyama Mang’ara kwa tuhuma za kukiuka Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Kiongozi huyo amefikishwa mbele ya Baraza la Maadili jana Jumatano, Januari 14, 2026 katika ofisi za Sekretarieti hiyo Jijini Dodoma akikabiliwa na mashtaka manne.

Wakili Mkuu wa Serikali, Hassan Mayunga ameliambia Baraza hilo kuwa Manyama bila sababu za msingi ameshindwa kutimiza matakwa ya kifungu cha 6(1)(a) na 6(1)(c) vya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma hivyo, kukiuka maadili ya uongozi wa umma kwa mujibu wa kifungu cha 6(2) cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

“Wakati akikaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe na akitekeleza majukumu yake aliwahamisha kituo cha kazi watumishi wawili wa halmashauri hiyo na kuwashusha vyeo.

Watumishi hao ni Asifiwe Chipata na Mercy Kabaka bila kuzingatia sheria.

Shtaka jingine ni kumpanisha cheo Mohamed na Edmund Kowi kuziba nafasi hizo.

Mtuhumiwa alikiri kutenda mashtaka hayo mbele ya Mwenyekiti wa Baraza hilo, Jaji Rose Teemba na kuomba kusamehewa kwa kukosa umakini ambako Baraza liliahidi kutoa uamuzi wake mara baada ya kupitia hoja zote.

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *