Wazazi wa wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangiwa shule za Serikali lakini wakaandikishwa shule binafsi wametakiwa kutoa taarifa katika shule walizopangiwa awali, ili Serikali iwe na kumbukumbu sahihi.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Divisheni ya Elimu ya Sekondari Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Musa Ally.