Zaidi ya wananchi 200 wa kijiji cha Kihangaiko, kata ya Msata, wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani, wamepata elimu ya tiba, huduma za matibabu, pamoja na msaada wa vyakula kutoka Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia Shule ya Mafunzo ya Awali ya Kijeshi (RTS) Kihangaiko.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Mkuu wa Shule hiyo, Sijaona Michael Myalla, amesema misaada hiyo imetolewa kama sehemu ya Zoezi la Medani “Exercise Maliza”, linalotekelezwa na kruti katika eneo la Msata.
Mhariri | @claud_jm
#azamtvupdates