Mchambuzi wa uchumi, Ally Mkimo, amesema mabadiliko ya kiwango cha riba cha Benki Kuu (CBR) yana mchango mkubwa katika kuleta athari chanya na hasi kwa jamii, kutegemea mwelekeo wa riba hiyo—iwe inapanda au kushuka.
Akizungumza kuhusu athari hizo, Mkimo amesema CBR inapokuwa chini, mzunguko wa fedha huongezeka kwenye uchumi, hali inayorahisisha upatikanaji wa mikopo na kuchochea matumizi.
Hata hivyo, ameonya kuwa hali hiyo inaweza kusababisha mfumuko wa bei iwapo ongezeko la fedha litazidi kasi ya uzalishaji wa bidhaa na huduma.
✍Halima Abdallah
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates